Michezo

Simba SC kuweka kambi Iringa kabla ya kuivaa Mtibwa Sugar

Mara baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 2 –  0 dhidi ya Njombe Mji mchezo uliyopigwa hapo jana siku ya Jumanne, kikosi cha Simba SC kimeanza safari yake asubuhi ya leo kuelekea Mkoani Iringa ambapo kinatarajia kuweka kambi yake siku mbili.

Vinara hao wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wataondoka Mkoani Iringa na kuwafuata wapinzani wao Mtibwa Sugar wenye maskani yao Mkoani Morogoro siku ya Ijumaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents