Tia Kitu. Pata Vituuz!

Simba ubingwa wa Ligi Kuu  ‘Ndiyo basi tena’, hatma ya yote kujulikana saa 24 zijazo

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, Wallace Karia ameeleza Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi kuu kuitisha kikao cha dharura kesho siku ya Jumatano ya Machi 18, 2020.

Image result for simba bingwa ligi kuu

Kikao hicho kitakachoanza saa 3:00 asubuhi, kitafanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, City Center Dar es Salaam.

Ajenda kubwa katika kikao hicho ni kuangalia mustakabali wa ligi kutokana na mlipuko wa Virusi vya ugonjwa wa Corona ambao umeingia nchini.

Kuna uwezekano mkubwa sana Shirikisho hilo kupitia kwa Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu kusimamisha michuano yote inayosimamiwa na chombo hicho chenye mamlaka ya soka nchini ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa huo hatari wa Virusi vya Corona.

Simba SC wakiwa watetezi wa ubingwa huo mara baada ya kuchukua mara mbili mfululizo ikiwemo sasa ndiyo inayoongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 71 juu kabisa ya msimamo wakati wanaowafuatia Azam FC wakiwa na alama 54 tofauti ya zaidi ya pointi 17 katika mzunguko huu wa pili na hivyo kupewa nafasi kubwa ya kuchukua taji hilo kwa mara ya tatu kama walivyowahi kufanya watani wao wa jadi ya Yanga SC.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW