Michezo

Simba wapigana vikumbo na Yanga Visiwani Zanzibar

Mabingwa wa FA, klabu ya soka ya Simba jioni ya leo inataraji kusafiri kwenda Visiwani Zanzibar kuweka kambi kwaajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Dar es salaam Young Africans utakao pigwa Agosti 13 mwaka huu.

Kikosi cha Timu ya Simba

Timu hiyo inakwenda Zanzibar kujiwinda na mchezo huo huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa tayari wamesha wasili Visiwani humo mara baada ya kucheza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo wa Yanga na Ruvu Shooting wahamia Chamazi

Simba ambayo imedhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa inaonekana kufanya vizuri katika usajili wake msimu huu kwa kuwasajili baadhi ya wachezaji golikipa Aishi Manula , beki Shomari Kapombe, mshambuliaji John Bocco wote kutokea Azam FC, Ammanuel Mseja, Ally Shomari, Saidi Mohamed, Haruna Niyonzima huku wa kifanikiwa kumrudisha mchezaji kipenzi cha mashabiki wa msimbazi Emmanuel Okwi.

Mbali na mchezo dhidi ya Yanga lakinipia klabu hiyo itatumia kambi hiyo kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambao unatarajia kuanza kutimuavumbi Agosti 26 mwaka huu.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents