Habari

Maporomoko ya ardhi yauwa watu 200

Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kufariki dunia baada ya maporomoko ya ardhi kutokea nchini Sierra Leone mapema leo asubuhi.

A picture of the mudslide
Eneo lililopatwa na maporomoko

Maporomoko hayo yametokea katika eneo moja la milima mjini Free Town kaskazini mwa nchi hiyo baada ya mvua kali kunyesha usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP ni miili 12 tu iliyopatikana kwenye kifusi cha udongo huku zaidi ya watu 200 wakihofiwa kufukiwa.

Mpaka sasa taarifa zilizotolewa na serikali nchini humo zinasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi ya watu waliofariki kwenye janga hilo.

Taarifa za kutokea janga hilo zilianza kusambaa mapema leo asubuhi kupitia mitandao ya kijamii ambapo wakazi wengi wa mji wa Free Town walituma picha mitandaoni zikionesha hali ya hatari baada ya mvua kali kunyesha na kusomba nyumba.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents