Michezo

Simba yakusudia kuifanyia kitu gani nembo yake  ?, yaacha swali hili kwa mashabiki

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sports Club wanatarajia kufanya maboresho ya nembo yao (logo).

Habari hiyo imewekwa wazi na Simba wenyewe kupitia akaunti zake za kijamii na kuwataka Wanamsimbazi kufanya chaguo ambalo wao wangependa.

”Hivi karibuni tutaanza utaratibu wa kufanya maboresho ya logo yetu. Kama Mwanasimba ungependa kuona mabadiliko yapi kwenye logo yetu ?,” – Simba SC.

Inafahamika kuwa klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1936, inatumia nembo yenye picha Mnyama Simba kama lilivyo jina lake, huku kwa juu kukiandikwa mwaka uliyoanzishwa timu hiyo kisha jina la timu.

Hata hivyo nembo hizi za Simba zipo mbili ambazo ndiyo maarufu zaidi, moja ikiwa nyeupe yenye maandishi yenye randi nyekundu na ya pili ni ile nyeusi .

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents