Burudani ya Michezo Live

Simba yaungana na Liverpool, Chelsea na Newcastle ”Black Lives Matter”

Miamba ya soka nchini Tanzania, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba Sports Club hii leo siku ya Jumatano nyota wake wamepiga goti moja wakati wa mazoezi katika viwanja vyake vya vya Bunju ikiwa ni ishara ya kupinga vitendo vya ubaguzi.

 

Kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi Simba kimeungana na klabu za England, ambapo hapo jana Chelsea na Newcastle zilifuata nyayo za Liverpool kuwa miongoni mwa klabu zinazotoka Premier League kupiga goti moja kama ishara ya kuunga mkono harakati za ‘Black Lives Matter’ kupinga ubaguzi wa rangi kufuatua kifo cha Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd.

Chelsea players took the knee in the H formation for 'human' during training on Tuesday

Kikosi cha Chelsea

Wachezaji kutoka katika klabu ya jiji la London walipiga magoti wakati wa mazoezi katika viwanja vya Cobham.

Mlindalango, Kepa ameelezea katika akaunti yake ya twitter kwa kuandika ujumbe kuwa inatosha, ”Inatosha, sisi sote ni binadamu. Pamoja tupo imara.”

Hatua hiyo imejitokeza pia kwa upande wa wachezaji wa klabu ya Newcastle ambao nao walipiga magoti wakati wa mazoezi katika kuunga mkono harakati za kupinga ubaguzi.

Wakati kikosi cha Liverpool siku ya Jumatatu kilipiga magoti kwa kuonyesha ishara ya umoja juu ya kifo cha Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi kabla ya kuanza mazoezi yake katika uwanja wa Anfield.

Wachezaji hao kila mmoja alikunja goti moja na kutengeneza duara katikati ya uwanja na kuitazama kamera iliyokuwa ikiwamwilika uwanjani hapo.

The Liverpool squad stopped training to show solidarity with the Black Lives Matter movement

Nyota hao wameonekana kuvalia jezi zenye rangi tofauti tofauti, wengine wakiwa na rangi nyeusi, nyeupe, nyekundu wakati wengine wakiwa wamevalia jezi za mazoezi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW