Michezo

Singida United washushiwa rungu na Kamati ya Saa 72

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi imeipiga faini klabu ya Singida United.

katika kikao chake kilichokaliwa na kamati hiyo kimeikuta na makosa timu hiyo kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi ya ligi kuu waliyocheza Aprili 11, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Yanga.

Kutokana na kosa hilo Singida amepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) za Kitanzania.

Wakati huo huo mchezaji Tafadzwa Kutinyu wa timu hiyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kutokana na kufanya vitendo vya kuonyesha imani za kishirikina katika mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Katika mchezo huo Kutinyu alichukua taulo la kipa wa Mtibwa Sugar na kulirusha jukwaani kwa washabiki wa Singida United ambao waliondoka nalo.

Bodi ya Ligi imepeleka malalamiko kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya Meneja wa Singida United, Ibrahim Mohamed kwa kuongoza vurugu za timu yake kulazimisha kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents