Singida United yaaga mashindano ya SportPesa Super Cup
Klabu ya Singida United imeyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuktolewa na timu ya AFC Leopard ‘Ingwe’ kutoka nchini Kenya kwa hatua ya mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo.
Wachezaji wa klabu ya Singida United
Singida United iliyopanda ligi kuu msimu huu ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Mzimbabwe Kutinyu Tafadzwa, kabla ya ‘Ingwe’ hawa wa Kenya kusawazisha kupitia kwa mchezaji wao Vincent Oburu.
Wachezaji wa klabu ya Singida United wakicheza na AFC Leopard katika mchezo wa kombe la SportPesa Super Cup
Baada ya kusawazisha timu zilicheza kwa kushambuliana kila moja kwa zamu na kosa kosa za hapa na pale hadi mchezio kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Wachezaji wa klabu ya Singida United wakicheza na AFC Leopard katika mchezo wa kombe la SportPesa Super Cup
BY HAMZA FUMO