Burudani

Snoop Dogg na Oprah Winfrey waizika beef yao iliyodumu kwa miaka 7

Mwaka 2007 malkia wa talk show Opray Winfrey alimshutumu rapper Snoop Dogg kuwa anahamasisha chuki dhidi ya wanawwake (misogyny) katika nyimbo zake, kitu kilichosababisha Snoop kuchukia na kutengeneza beef ambayo imezikwa rasmi Ijumaa hii.

oprah n snoop

Mastaa hao walikutana katika sherehe ya Oscars huko Los Angeles, Marekani Ijumaa usiku na kuthibitisha kumaliza tofauti zao kwa kupiga picha pamoja wakiwa na furaha.

Snoop alipost picha hiyo Instagram na kuandika ‘Black History’.

Mwaka 2007 Oprah aliendesha kipindi kilichokuwa kinazungumzia ‘misogyny’katika muziki wa Hip Hop na kumtaja Snoop kuwa mmoja wa watuhumiwa wakubwa.

Kilichomuudhi Snoop ni kuwa hakupewa nafasi ya kuja kwenye kipindi na kujitetea hivyo kuanzia hapo ndipo alianza kumchukia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents