Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Soka la ufukweni kuanza kesho Dar

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limeandaa ligi ya soka la ufukweni kwa vyuo vya Mkoa wa Dar es Salaam mashindano yanayopangwa kuanza kesho Novemba 18, 2017.

Ligi ya mwaka huu itafanyika katika viwanja vya Escape One – Mikocheni uliopo Wilaya ya Kinondoni na itajumuisha jumla ya timu 16.

Mpaka sasa maandalizi yanaendelea kwa mafanikio makupwa kupitia dawati la soka la ufukweni na futsal “soka la sakafuni”

Mafunzo kwa waamuzi wapya

Kabla ya kuanza ligi hiyo kesho, TFF iliendesha mafunzo mafupi ya waamuzi kutoka Novemba 5 – 11, 2017 kwa lengo la kupata waamuzi wapya watakaosaidia na wengine waliyopo katika kuendesha mashindano hayo.

Timu zote 16 zimegawanywa katika makundi mawili.

Kundi A litakuwa na timu za DMI, SIBM, TPSC, MNMA, CBE, AMCET, TIA, IFM na Kundi B litakuwa na timu za DIT, LBC, ARDHI, DSJ, TUMAINI, NIT, UAUT, HKMU.

Kila kundi likiwa na timu nane na timu zote katika hatua ya makundi zitacheza mechi mojamoja na kila timu katika kundi lake.

Michezo imepangwa yote kufanyika uwanja wa Escape one kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku ya Jumamosi na Jumapili kuanzia Novemba 18, mpaka Desemba 9, 2017.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW