Michezo

SportPesa: Mfahamu kiungo wa Everton anayewanyima usingizi Gor Mahia

Kuelekea Julai 13 katika mchezo wa kirafiki kati ya klabu ya ligi kuu ya nchini Uingereza, Everton dhidi ya mshindi wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia, mashabiki wa soka nchini wanasubiria kuwashuhudia ‘live’ wachezaji mbalimbali wa klabu hiyo iliyoshika nafasi ya 7 katika msimu wa ligi 2016/17.

Bongo5 itakuwa inakuletea uchambuzi mbalimbali kuelekea mchezo huo ambapo Jumanne hii tumekuletea profile ya mmoja kati ya viungo wa timu hiyo, Morgan Schneiderlin ambaye huwenda akatua nchini na klabu hiyo inayodhaminiwa na kampuni kubashiri ya SportPesa katika hatua za kujiweka sawa dhidi ya mikikimikiki ya ligi kuu msimu ujao.

Morgan Schneiderlin amejiunga na klabu ya Everton mwezi Januari 2017 akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja wa klabu hiyo, Ronald Koeman.

Schneiderlin akiwa na kocha wake,Ronald Koeman

Mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, aliwasili klabuni hapo akitokea Manchester United kwa mkataba wa miaka minne na nusu kwa ada ya £ 24 millioni.

Schneiderlin alihamia Goodison Park baada ya kuisaidia timu yake ya zamani Manchester United kuchukua ubingwa wa kombe la FA Cup katika mchezo uliofanyika Wembley Mei 2016.

Schneiderlin kwa mara ya kwanza alifika England Juni 2008 baada ya kusajiliwa na klabu ya Southampton akitokea katika klabu ya academy Strasbourg ya nchini Ufaransa.

Msimu wa kwanza wa Schneiderlin na Southampton ulimalizika kwa kukata tamaa baada ya timu yake hiyo kufanya vibaya katika michuano ya League  One.

Lakini baada ya kukaa ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya miaka sita, aliweza kuonyesha makali yake ndani timu hali iliyopelekea klabu kubwa mbalimbali ikiwemo Manchester United kuanza kumtamani.

Akiwa na Southampton alicheza michezo 42 ya League One mwaka 2011/12 na baada ya miaka michache baadaye timu yake hiyo iliweza kupanda ligi kuu.

 
Schneiderlin aliendelea kuwa mchezaji muhimu wa Southampton chini ya kocha Mauricio Pochettino hali ambayo ilimpelekea kutajwa kuwa mchezaji bora wa wakuchaguliwa na wachezaji wenzake katika msimu huo.

Juhudi za Schneiderlin zilizaa matunda zaidi baada ya kuonyesha uwezo mkubwa ndani ya ligi ya Uingereza hali iliyopelekea kuchagulia na kuingia kwenye timu ya vijana ya Ufaransa.
 
Hatua hiyo ilimfanya Schneiderlin kuwa katika kikosi cha Didier Deschamps kilichoshiriki Kombe la Dunia nchini Brazil, ambako alicheza mara moja dhidi ya Ecuador.
 
Katika msimu wa mwaka 2014/15, Southampton ilipata nafasi ya kushiriki Europa League baada ya kumaliza nafasi ya saba Ligi Kuu.

Kwa sasa Schneiderlin amekuwa ni mmoja kati ya wachezaji wa muhimu wa kikosi cha kwanza cha Everton ambacho kinatarajiwa kutua nchini Tanzania mwezi Julai.

Mashabiki wa soka nchini wasubiria kwa hamu kumuona kiungo huyo mahiri akiwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakati timu yake ikichuana na mshindi wa timu ya SportPesa Super Cup Gor Mahia ya nchini Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents