Michezo

Stars wa Harambee na Taifa kuzichapa

 


Timu ya Taifa ya Kenya,Harambee Stars inatarajia kuingia nchini Jumapili jioni  kushuka dimbani kwa mechi ya kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania, Kilimanjaro Stars,


siku ya  Jumatatu ijayo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kupimana nguvu kabla ya kuingia katika msahindano ya Tusker CECAFA yanayotarajiwa kuanza mapema Desemba mwishoni mw mwaka huu.

Bw. Sunday Kayuni, katibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,TFF, alisema, ‘Timu ya Harambe Star inatarajia kuwasili nchini Tanzania Jumapili jioni  wakijiandaa kwa mchezo huo wa kirafiki utakaochezwa jumatatu.

Kayuni aliongeza kwa kusema kuwa huo ni mchezo wa kirafiki na unafuata taratibu za shirikisho la mpira wa miguu FIFA na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo itawaandalia mazingira mazuri ya kujua uwezo wao uko wapi.

Aidha Kayuni alimalizia kwa kusema kuwa ilishindikana kupata timu ya kucheza na Kilimanjaro Stars kupimana uwezo hivyo kuamua kuichukua Harambe Stars  kucheza nao mpira wa kirafiki ili kupata mazoezi zaidi  kujiandaa katika mtanange uliopo mbele yao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents