Michezo

Stephen Curry ndiye mshindi MVP wa NBA msimu huu

Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry achaguliwa mchezaji bora wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) msimu huu.

3403AA7E00000578-0-image-m-2_1462906552401

Stephen Curry mwenye umri wa miaka 28 alichaguliwa MVP msimu huu kutokana na mchango wake mkubwa wa kuiletea ushindi timu yake katika mechi 73 na kuweka rekodi.

Mafanikio ya Stephen Curry yamemfanya kuwa mchezaji wa 11 kuwahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwa misimu miwili mfululizo.

Wachezaji wengine waliowahi kuchaguliwa MVP mara mbili mfulululizo ni Karim Abduljabbar, Bill Russell, Wilt Chamberlain, Michael Jordan, Moses Malone, Larry Bird, Magic Johnson, Tim Duncan, Steve Nash na LeBron James.

Ameweka rekodi ambayo haikuwahi kufikiwa na magwiji walio pita katika mchezo huo na NBA kama Magic Johnson, Michael Jordan na LeBron James.

Curry ambaye ni mlinzi wa timu ya Golden State Warriors, amebeba kura zote 131 kupata ushindi huo, jambo ambalo halikuwahi kutokea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents