Tupo Nawe

Studio ya Nahreel ‘The Industry’ yamtambulisha rasmi msanii mpya wa label yao, Rosa Ree

Studio ya The Industry inayomilikiwa na producer Nahreel, imemtambulisha rasmi msanii mpya aitwaye Rosa Ree atakayekuwa chini ya label yao kuanzia January 14, 2016.

ROSA REE 1

Rose Ree mwenye miaka 20 ni rapper wa kike ambaye kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi kuanzia sasa katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni za Tanzania na nje ya nchi.

Hii ni hatua nyingine kwa founder na mtayarishaji wa studio hiyo Nahreel ambaye pia ni msanii wa kundi la Navy Kenzo, katika kutimiza ndoto yake ya kuupigisha hatua muziki wa Tanzania kwa kusaidia vijana wengine wenye vipaji.

Miezi michache iliyopita The Industry pia ilianzisha chuo cha muziki ‘TIMS’.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW