Michezo

Tamko la LaLiga kuhusu Lionel Messi kuondoka, yataja vifungu vya sheria

Tamko la LaLiga kuhusu Lionel Messi kuondoka, yataja vifungu vya sheria

Madrid, 30 Agosti 2020 – Shirikisho la soka nchini Hispania, LaLiga limesema kuwa limefuatilia kwa karibu taarifa zilizokuwa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari kuhusu Mkataba wa mchezaji, Lionel Andres Messi na klabu ya FC Barcelona na baada ya kuupitia kandarasi hiyo, LaLiga imeona ipo haja ya kufafanua juu ya swala hilo.

La Liga Confirm Lionel Messi's €700 Million Release Clause Has NOT Expired - SPORTbible

  • Mkataba unaotumika sasa una kipengele cha ‘release clause’ ambacho kitatumika kama, Lionel Andres Messi ataamua kukatisha kandarasa yake mapema kwa mujibu wa kifungu cha 16, amri ya Kifalme (Royal Decree 1006/1985 ya Juni 26) kwa sheria za Hispania ambayo ndiyo husimamia kazi za taaluma ya wanamichezo.

 

  • Sambamba na kanuni na utaratibu unaotumika katika visa kama hivyo, LaLiga haitaendelea na kutolewa kwa mchezaji anayehitajika kufutiwa usajili kutoka kwa Shirikisho la Soka la Uhispania isipokuwa kifungu kilichotajwa hapo awali kimeshalipwa.

Kwa maana hiyo basi ‘release clause’ bado inafanya kazi ni tofauti na yeye Messi anavyoamini kuwa anaweza kuondoka pasipo hiyo kutokana na sehemu ya mkataba wake kuwepo makubaliano yanayomruhusu kuondoka kama atahitaji kufanya hivyo kila ifikapo mwisho wa msimu.

Inaelezwa kuwa Lionel Messi Jumapili hii hakwenda kufanyiwa vipimo vya Corona ndani ya Barcelona ili kuwa tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents