MichezoUncategorized

TANZIA: Mtoto shabiki namba moja wa Sunderland afariki dunia

Shabiki namba moja wa klabu ya soka ya Sunderland ya Uingereza, mtoto Bradley Lowery amefariki dunia.

Mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka sita alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa muda mrefu hali iliyofikia mpaka madaktari kutangaza kushindwa kumtibia kwa madai kuwa tayari imeshafikia katika hali mbaya. Madaktari hao walidai kuwa Jumamosi ya February 11 ya mwaka huu ndio ungekuwa mwisho wa Bradley kuishi duniani lakini jambo hilo halikuwa kama walivyofikiria.


Mtoto Bradley Lowery akiwa na mama yake mzazi Gemma Lowery

Mwanzoni kabla ya madaktari hao kutangaza kushindwa kutibu Lowery, ilidaiwa kuwa matibabu ya mtoto huyo yatagharimu kiasi kisichopungua bilioni mbili ambapo timu za Everton, Man City na Sunderland pamoja na wadau wengine walijitolea kumchangia lakini baadae jopo la madaktari lilitoa taarifa ya kushindikana kwa matibabu hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents