Technology

Tecno Phantom 9 yazinduliwa rasmi Tanzania, Yaja na sifa za kipekee (+video)

Kampuni ya simu nchini ya TECNO imezindua rasmi simu yao kubwa ya TECNO Phantom 9 ikiwa ni mwendelezo katika matoleo ya Phantom ikiambatanishwa na ofa ya GB 18.

TECNO Phantom 9 ni simu ya kwanza katika upande wa TECNO Phantom series kuja na kamera tatu za teknolojia ya AI (AI triple) zenye 16MP+8MP+2MP.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa Uhusiano wa kampuni ya TECNO, Bwana Eric Mkomoye amesema kwamba “Katika ulimwengu wa sasa wa smartphone, kamera zinapata ushindani mkubwa toka kwa kamera za simu kwani kila mpiga picha anatambua umuhimu wa kutumia simu yenye kupiga picha vizuri ili kuepuka usumbufu wa kujibebesha mizigo, na TECNO tumelifanyia kazi kupitia Phantom 9 kwani ina kila sifa zenye kukidhi haja ya wateja wetu wanaopenda kuchukua matukio kupitia kamera za simu zao.”

Bwana Mkomoye aliongeza kuwa “TECNO phantom 9 ikiwa kama flag ship ya kampuni kwa mwaka huu, TECNO imehakikisha ujuzi si katika upande wa kamera tu bali hata uwezo wa kuhifadhi files na speed ni mkubwa ikipewa uwezo na memory yenye GB 128Rom + 6Ram pamoja na Operating system ya Android Pie (P). “Lakini vile vile phantom 9 ina AMOLED Screen ya nch 6.4 FHD yenye kupiga picha zenye rangi halisi na upana zaidi”. .

Naye muigizaji wa filamu, Gabo akiongea kama balozi wa toleo hilo la simu, Amesema simu hiyo imekujja kuleta mapinduzi kwenye masoko ya simu hapa Tanzania, kwani ina vitu vyote muhimu na inauzwa kwa bei rahisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents