Picha

Tetesi za daktari wa Michael kuwa baba wa watoto wake (MJ) zaibuka tena!

Dame Elizabeth Taylor Diamond Jubilee Birthday

Ingawa hayati Michael Jackson alidai kuwa aliwazaa watoto wake wote watatu, kumekuwepo na tetesi za siku nyingi kuwa alitumia ‘sperm donor’ (kutumia mbege za wanaume wengine).

Na sasa daktari wake wa zamani Dr. Arnold Klein, ameibuka na kusema kwa ‘mafumbo’ kuwa yeye ndio baba mzazi wa mtoto wa Michael mwenye miaka 15, Prince Michael.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Klein alipost picha yenye fumbo kwenye ukurasa wake wa Facebook Jan. 17, inayoonesha jinsi Prince Michael anavyofanana na Klein alipokuwa mdogo na kuiandikia maneno “hmmmmm.”

Klein

Klein alidaiwa kuwa ni baba wa mtoto huyo mkubwa wa kiume wa Michael na wa kike Paris, kwasababu Jackson alikutana na mke wake wa zamani Debbie Rowe (ambaye ni mama watoto hao wawili) alipokuwa akifanya kazi kwenye ofisi ya Klein.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents