Aisee DSTV!

Tetesi za soka barani Ulaya: Guardiola kupumzika katika soka, United wafanya mawasiliano na kiungo wa Barcelona 

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaangalia uwezekano wa kuchukua mapumziko ya muda katika soka mwishoni mwa msimu ujao ikiwa atashinda Championi Ligi . (Star)

Manchester United wamefanya mawasiliano na kiungo wa kati wa Barcelona Mcroatian Ivan Rakitic mwenye umri wa miaka 31. (Sport – in Spanish)

United watatakiwa kuvunja mikataba miwili ya rekodi ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya ulinzi, ikiwa watahitaji kusaini mkataba na wachezaji wa safu hiyo kutoka England Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Crystal Palace na Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Leicester watakaolipwa pamoja pauni milioni 130. (Standard)

Hata hivyo , United wanataka sana kusaini mkataba na mchezaji wa timu ya England ya Norwich City anayecheza safu ya ulinzi Max Aarons,mwenye umri wa miaka 19, ikiwa azma yao ya kumchukua Wan-Bissaka itafanikiwa. (Sky Sports)

Mlinzi wa klabu ya Ajax ya Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, anasema ” hajui moyo wake unasema nini ” lakini ataamua juu ya hali yake ya baadae atakapokuwa mbali likizoni . (Mundo Deportivo – in Spanish)Chelsea wameanzisha mazungumzo na meneja wa Derby Frank Lampard juu ya kurejea katika Stamford Bridge

Chelsea wameanzisha mazungumzo na meneja wa Derby Frank Lampard juu ya kurejea katika Stamford Bridge

Washauri wa De Ligt wamemwambia aende katika timu kama Manchester United ambako anakuwa na hakikisho la kuanza , kabla ya kuhamia Barcelona baadae katika taaluma yake (Sport)

Chelsea wameanzisha mazungumzo na meneja wa Derby Frank Lampard juu ya kurejea katika Stamford Bridge kwa kiungo huyo wa zamani wa kati wa Blues.(Mail)

Chelsea wanataka Meneja atakayechukua nafasi ya Maurizio Sarri anayeongoza timu hiyo ambaye tayari anatarajia kuhamia katika klabu ya Italia ya Juventus baadae wiki hii. (Mirror)

Real Madrid watafanya kila wawezalo kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, mwenye umr wa miaka 26, kwani ndio chaguo la kwanza la Zinedine Zidane (Marca)

West Ham wanamlenga mchezaji wa safu ya kati ya timu ya Villarreal ya Uhispania Pablo Fornals, mwenye umri wa miaka 23, Baada ya kutuliza haja yao kwa kiungo wa kati wa Celta Vigo Mslovakia Stanislav Lobotka, mwenye umri wa miaka 24. (Guardian)

Mlindalango wa Utaliano Gianluigi Buffon, mwenye umri wa miaka 41, anaweza kujiunga na Porto baada ya kuondoka Paris St-Germain, kuchukua nafasi ya Spaniard Iker Casillas, mwenye umri wa miaka 38. (Tuttosport – in Italian)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW