Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi hii, Barcelona yamuandalia dau Willian, Solskjaer kumsajili Moussa Dembele

Klabu ya Barcelona inaanda dau la pauni milioni 30 ili kumsajili mchezaji wa Chelsea raia wa Brazil Willian mwenye umri wa miaka 30. (Sun)

Willian

Manchester City imefanya mkutano na wazazi wa beki wa Benfica joao Felix 19 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United na Liverpool. (Record, via Express)

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameanzisha harakati zake za kumsajili mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 22. (L’Equipe, via Mirror)

Chelsea itaanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 23, kuhusu mkataba mpya . (Sun)

DembeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mchezaji wa Paris St-Germain aliyesainiwa kwa rekodi ya dunia Neymar, 27, huenda akauzwa kwa dau la £145m mwisho wa msimu huu kutokana na sheria inayomzuia kuuzwa . (Mundo Deportivo, via Mirror)

Mkufunzi wa Tottenham Mauuricio Pochettino ameonya Tottenham kwamba atalazimika kufanya mabadiliko yenye ‘uchungu’ mkubwa ili kuimarisha klabu hiyo kuwa katika kiwango cha uwanja mpya. (London Evening Standard)

Rodriguez

Mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich, atauzwa kwa dau la £36m na Real Madrid mwisho wa msimu huu na klabu za Manchester United na Chelsea huenda zina hamu ya kumsajili mchezaji huyo.27. (Marca, via Express)

Rafael Benitez amesema kuwa anakaribia kusalia katika klabu ya Newcastle na huenda akaandikisha kandarasi mpya inayokamilika mwezi ujao.. (Guardian)

Mchezaji wa Argentina anayelengwa na Arsenal Nicolas Tagliafico, 26 ametangaza kwamba atasalia na klabu ya Ajax kwa msimu mwengine. (Football.London)

Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaREUTERS

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amefichua kwamba ataamua ni wachezaji gani atakaowasajili na anasisitiza kwamba klabu hiyo inamvutia mchezaji yeyote yule. . (Talksport)

Beki wa Chelsea David Luiz amefanya mazungumzo mapya na klabu hiyo kuhusu kuandikisha kandarasi mpya ili kuongeza uwepo wake katika klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 huenda akaondoka katika uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu wakati kandarasi yake itakapokamilika. (London Evening Standard)

Fernando LlorienteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 34, yuko tayari kuongeza kandarasi yake katika klabu hiyo kwa msimu mwengine.. (Sky Sports)

Ajenti wa mshambuliaji wa Stoke Saido Berahino anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anafikiria kusitisha kandarasi yake na klabu hyo ili kujiunga na klabu ya Fenerbahce. (Express and Star)

Mshambuliaji wa Leeds Caleb Ekuban, 25, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa dau la £2m kuelekea katika klabu ya Uturuki baada ya kutangaza kwamba huenda akasalia katika klabu hiyo kupitia kandarasi ya kudumu. (Yorkshire Post)

Mkufunzi wa Birmingham Garry Monk amepinga uvumi unaomuhusisha na West Brom. (Birmingham Mail)

Mkufunzi wa klabu ya Brighton Chris Hughton hana mpango wa kutazama mechi muhimu ya EPL kati ya mahasimu wao wanoashushwa daraja Cardiff na Crystal Palace ambayo huenda ikaifanya klabu yake kusalia katika ligi ya kuu ya Premia. (Argus)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents