Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili hii, United yampa siku 7 De Gea, Barca yatangaza kitita kinono cha fedha kumng’oa Lacazette, Zidane amkana Pogba 

Mlindalango wa kimataifa raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 28, David de Gea amepewa wiki moja ili kuamua mustakabali wake na klabu yake ya Manchester United. (Sun)

David De Gea

Miamba ya soka ya Hispania Barcelona imetangaza dau nono na la kushtukiza la pauni milioni 70 ili kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa mwenye umri wa miaka 27, Alexandre Lacazette. (Sunday Express)

Manchester United wanaweza wakapewa nafasi ya kumsajili kipa wa Real Madrid Keylor Navas, 32, katika kipindi hiki ambacho hawana uhakika endapo De Gea atasalia klabuni hapo. (Telegraph)

Chelsea wametakiwa kuheshimu makubaliano waliyoingia na mshambuliaji wao Eden Hazard ya kuwa ili ajiunge na Real Madrid, alitakiwa kusalia klabuni hapo msimu huu na pale utakapoisha ataruhusiwa kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania. (Sun)

Manchester City wanajipanga kuchuana na Barcelona katika mbio za kumsajili beki na nahodha kinda wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, mwenye thamani ya pauni milioni 65. (Star)

Matthijs de Ligt
Image captionMatthijs de Ligt

Kiungo wa Manchester United Juan Mata yawezekana akarejea Uhispania msimu ujao – huku klabu ya Athletic Bilbao ikimuwania kiungo huyo mwenye miaka 31 kwa udi na uvmba. (Mirror)

Zinedine Zidane amekana kuhusishwa na uvumi juu ya uhamisho wa wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba 26, kwenda Real Madrid. (Manchester Evening News)

Paul Pogba
Image captionPogba kuihama Man United? Jibu litapatikana siku chache zijazo dirisha la usajili likifunguliwa.

Pogba ameambiwa kuwa hatapata nafasi nyengine tena ya kuhamia Madrid endapo hatafanya hivyo mwishoni mwa msimu huu. (Sun)

Beki wa Atlanta United Florentin Pogba, 28, ambaye ni kaka wa Paul, anaamin: “kuna kitu kitatokea majira haya ya kiangazi” na amekataa kusema iwapo mdogo wake hatohamia moja wapo ya klabu kubwa za Uhispania Real Madrid ama Barcelona for his sibling. (AS, via Calciomercato)

Mourinho
Image captionMourinho alitimuliwa kazi na Machester United mwezi Disemba

Kocha aliyetimuliwa kazi na Manchester United Jose Mourinho, 56, amepatiwa ofa ya kuifundisha klabu ya AS Roma kwa miaka mitatu, lakini atajiunga na klabu hiyu endapo watafuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya. (L’Equipe, via Mail on Sunday)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameahidiwa na uongozi wa klabu hiyo kuwa atawezeshwa ili afanye usajili mkubwa hivi karibuni. (Sun)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents