Michezo

TFF yamfungia Juma Nyoso kucheza soka kwa miaka miwili

Kamati ya uendeshaji ya ligi kuu Tanzania Bara iliyokutana September 29 kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini, imemfungia nahodha wa Mbeya City, Juma Nyoso kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili.

Juma-Nyosso

Pia imempiga faini ya shilingi milioni mbili kuafutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC, John Bocco.

Beki huyo wa Mbeya City alirudia tena kitendo hicho cha kuwadhalilisha wachezaji wenzake wake uwanjani kiasi ambacho TFF imeahidi kumchukulia hatua kali zaidi awamu hii.

“Udhalilishaji uliofanywa leo na mchezaji mmoja wa timu ya ligi kuu tumeuona,hatua kali zitachukuliwa muda sio mrefu,tuwe na subira,” Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliandika kwenye Twitter.

Nyoso amewahi pia kumfanyia kitendo hicho mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri na TFF kumwadhibu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents