Burudani

Nicki Minaj kutayarisha na kuonekana kwenye tamthilia ya maisha yake

Nicki Minaj anatarajiwa kuwa mtayarishaji mkuu wa tamthilia mpya kupitia ABC Family itakayoangaza maisha ya rapper huyo alivyokulia kwenye viunga vya Queens, New York.

nickiminaj

Mradi huo kutoka Kapital Entertainment, utatengeneza episode ya kwanza mwaka huu.

Tamthilia hiyo inaandikwa na Kate Angelo (Sex Tape), na itaangaza maisha ya Minaj aliyekulia Queens miaka ya 1990 pamoja na familia yake, alivyoanza muziki hadi kuwa maarufu.

Kabla ya kuwa staa, Minaj amewahi kusomea muziki kwenye shule ya kifahari, LaGuardia High School ya Manhattan.

Amewahi kuigiza kwenye filamu kama Ice Ace: Continental Drift kwa kuingiza sauti, filamu ya The Other Woman na hivi karibuni aliigiza kwenye filamu ya Ice Cube, Barbershop 3.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents