Burudani

Ben Pol ataja sababu 3 za kuachia wimbo mpya katika kipindi hiki cha uchaguzi

Wakati wasanii wengi wakiogopa kuachia nyimbo mpya katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuhofia kutopata muda wa kusikilizwa, Ben Pol ameeleza sababu zilizomfanya kutohofia kufanya hivyo.

11296894_150104848669823_348330056_n

Ben Pol aliyeachia wimbo ‘Ningefanyaje’ aliowashirikisha msanii wa Kenya, Avril na Rossie M ametaja sababu tatu za kuachia wimbo huo.

“Moja sina wimbo official tangia mwaka umeanza,” amesema Ben. “Nimetoa Sophia mwezi wa kwanza na sasa hivi ni mwezi wa tisa. Mbili napanga kufanya video na matarajio yangu ya video yanasema ni mwezi ujao mwishoni, kwa sasa siwezi kukaa kipindi chote hiki bila material mpya kwenye radio,” Ben Pol alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

“Halafu tatu huu wimbo ambao nimeutoa, nimeuperform kwenye Coke Studio season 3, na season 3 inaweza kuruka tarehe 10 October ni mwezi ujao kama wiki tatu. So nimeona ni bora wakati nauperform wimbo watu waujue na pia waweze kuupata kwa kuununua kwenye mitandao. Kwahiyo ndio maana nimeutoa huu wimbo kipindi hiki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents