Picha

THT yatembelea watoto wanaotibiwa kansa Muhimbili

Wasanii wa THT wakiwa na picha ya pamoja na watoto.
Wasanii wa THT wakiwa na picha ya pamoja na watoto.
Wasanii wa nyumba ya vipaji Tanzania (THT), jana walitembelea watoto wanaopata matibabu ya kansa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ili kuwafariji na kuwapa moyo wa kuendelea na matibabu ya ugonjwa huo.
Ziara hiyo ambayo ilijumuisha wasanii wote wa nyumba ya vipaji kama Ditto, Mwasiti, Barnaba, Amini, Linah, Makomando, Ali Nipishe, Mataluma na The Trio, iliwapa fursa watoto kuzungumza na wanamuziki hao wanaowapenda pamoja na kupata burudani ya muziki kutoka kwao.
Amini na Fred wa Makomando wakiwa na watoto (3).
Amini na Fred wa Makomando wakiwa na watoto (3).
Watoto hao ambao wanaishi katika hosteli na familia zao, wako chini ya taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa Tumaini la Maisha Tanzania ikihudumia zaidi ya kaya ishirini na nne.
Wakizungumza hospitalini hapo baada ya kuwaona wagonjwa hao, msanii Ditto alisema wameamua kutoa muda wao ili kuwafariji watoto hao kama mchango wao kwa jamii.
Linah akiimba na mtoto
Linah akiimba na mtoto
‘Ugonjwa wa kansa ni tatizo kubwa katika jamii yetu na ndio maana sisi kama THT tumeamua kuja hapa kuonyesha tunawajali na wao ni sehemu ya jamii yetu hivyo wasijisikie wametengwa’ alisema Ditto.
Barnaba na Linah wakiwaimbia watoto.
Barnaba na Linah wakiwaimbia watoto.
Nao watoto wanaopata matibabu hospitalini hapo walipongeza wasanii wa THT kwa kuwakumbuka, huku wakiomba wasanii wengine na jamii isiwasahau.
Muki, Mwasiti na Linah wakiimba.
Muki, Mwasiti na Linah wakiimba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents