Habari

TLC watoa sababu za kuondoa verse ya Left Eye katika version mpya ya ‘Water falls’

Siku 5 zilizopita kinadada wa kundi la TLC walitoa version mpya ya moja ya hit songs za kundi hilo za miaka ya 90 “Water falls” na ile verse ya rap ambayo katika original aliifanya marehemu Lisa ‘Left Eye’ Lopez walimuweka msanii wa kike kutoka Japan aitwaye Namie Amuro.

1995 MTV Movie Awards

Kitendo hicho kiliwakwaza wanafamilia ambao ni mama mzazi wa Left Eye pamoja na dada yake waliodai kuwa hawakuwa na taarifa mpaka walipokuja kushtukizwa na wimbo huo ukiwa tayari kwenye mtandao ukiwa hauna verse ya mpendwa wao Left Eye.

T-Boz na Chili members wa TLC waliobakia wameieleza TMZ kile kilichotokea. Cha kwanza wamedai kuwa kundi lao halina haki miliki za verse ya Left Eye katika wimbo huo, na maombi yao ya kupata haki hizo yalikataliwa, na kuongeza kuwa walilazimika kubuni njia nyingine ya kumuenzi mwenzao Lisa na kusheherekea 20th anniversary ya TLC na mashabiki wao, “We were forced to use a creative way to honor Lisa’s memory and celebrate this milestone with the fans.”

Kuhusiana na malalamiko ya mama na dada wa Left Eye kutohusishwa wala kupewa taarifa juu ya wimbo huo, TLC walisema walimtafuta Ron Lopez ambaye ni kaka wa marehemu Lisa kabla hawajatoa version mpya ya ‘Water Falls’.

TLC wameongeza kuwa siku zote wamekuwa na wataendelea kuilinda heshima ya dada yao Left Eye kwasababu TLC inaundwa na wao watatu akiwemo marehemu hivyo hapawezi kuwa na replacement ya Lisa wala member yeyote wa TLC, “We have and always will protect our sister’s legacy as TLC consists of the three of us collectively … there will never be a replacement for Lisa or any members in TLC.”

Kama hukupata nafasi ya kuisikiliza version mpya ya ‘Water falls’ isikilize hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents