TechnologyVideos

Toyota watia mkono kwenye utengenezaji wa Gari inayopaa (+Video)

Kampuni ya kuunda magari ya Toyota kutoka Japan imetangaza kuunga mkono kundi la waandisi ambalo linaunda gari linaloruka kwa kufadhili.

Picha inayohusiana
Mfano wa Gari linaloruka

Toyota imetoa kiasi cha Dola 300k za Kimarekani kwa kundi hilo ambalo huendesha shughuli zake nje ya mji wa Toyota nchini Japan.

Kundi hilo limekuwa likipata michango kugharamia kuundwa kwa gari hilo linalotumia teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na linatajwa kuwa gari dogo zaidi linaloruka kuwahi kuundwa.

Uharaka wa kuundwa kwa Gari hilo linalopaa unavaliwa njuga na makampuni mengi nchini Japan kwani matarajio ya kundi hilo la wataalamu wanataka magari hayo yatumike kwenye tukio la kuwasha Mwenge wa Michuano ya olimpiki mwaka 2020 mjini Tokyo,Japan .

Tazama mfano wa Video za Gari hilo jinsi litakavyofanya kazi

https://youtu.be/5YU8q6a5z1s

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents