Tuliwapapasa Ndanda FC wakacheza sindimba wakubwa Yanga SC wajiandae – Masau Bwire

Kufuatia kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Ndanda FC, Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kuifunga timu hiyo kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaoni ni kitendo cha furaha kwao na sasa wamewapatia kibali cha kuwapapasa watakao kuja mbele yao na kuwataka Yanga SC kuwamakini kwakuwa vijana wao wanahamu nao.

Kauli ya Masau Bwire inakuja baada ya timu yake ya Ruvu Shooting kuwa na mwenendo mzuri kwenye mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara kwakupata matokeo ya ushindi mfululizo.

Audio: Masau Bwire amtaka kocha wa Barcelona kuja Tanzania kujifunza kwa Ruvu Shooting

Ilikuwa raha na furaha watu wanapapaswa wanacheza sindimba raha kubwa kwelikweli uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Wakati tunaingia  tulipokelewa kwa maneno ambayo yalikuwa yanatoa hamasa kwa vijana wa Nangwanda vijana wa Ndanda FC wakisema kwao neno kupapaswa ni tusi na kuwataka wachezaji wao wahakikishe hawapapaswi sisi tukapata taarifa tukasema leo wamakonde humu ndani watakufa wengi kwa sababu tutawapapasa.

Walituita sisi walinzi wa Dangote sisi Ruvu Shooting, mbaya zaidi wakatufananisha na Mbwa kweli walitutia karaha na sisi tukawatumia salamu vijana wetu vijana wakasema ngoja sasa tuwaonyeshe kazi ilivyo zilianza pasi za kiulaya ulaya Ndanda FC wakachanganyikiwa wakapotea na kuusindikizampira tu kwa macho.

Tulipata goli letu la kusawazisha dakika ya 20 kupitia kwa mchezaji wetu Baraka Mtuli na tukaendelea kuonyesha uwezo wa kuchezea mpira dakika ya 27 tukapata bao la pili na dakika ya 42 tukaandika goli la tatu ndipo tukaamua kuacha kuwapapasa kwakuwa walisha sema kuwa kwao nineno baya tukaamua kuuchezea mpira dakika 90 zilivyomalizika wale waliyosema kupapaswa kwao ni tusi wakaja wakasema kweli wamepapaswa.

Ushindi huu unaonyesha namna tulivyojipanga malengo yetu tunayoyahitaji tuyafikie, kila mtu tunaekutananae mbele yetu lazima tumpapase na kwa sababu wamakonde hawa wametupa kibali cha kupapasa huyu mkubwa wa pale Jangwani ajipange vijana wanahamu naye sana na kasi tuliyonayo kwa sasa ni kubwa.

Matokeo ya mechi za jana siku ya Jumatatu ligi kuu soka Tanzania Bara

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW