MahojianoVideos

Tundaman: Nahisi Chidi Benz amekataa tamaa kufanya muziki


Hivi karibuni msanii wa Bongo Flava, Tundaman aka Captain, alitangaza kuwa msimamizi wa kazi za rapper Chidi Benz. Akiongea na Bongo5, Tundaman amesema aliamua kuwa meneja wa rapper huyo baada ya kumuona kama amekata tamaa na kufanya muziki.

“Nahisi sasa hivi kama Chidi Benz amekata tamaa ya kuchana na ni bonge la rapper, kwahiyo nimemuomba tu ili niweze kusimamia hizi kazi zake mbili tatu za kufanya audio, kufanya video na kujua kipi kinatoka kipi kinaingia. Mimi ndio mtu wa kwanza kumshauri na kusimamia hilo suala pia. Nashukuru yeye mwenyewe pia amekubali mimi ndio niwe namsimamia. Pia nimesikia faraja kwakuwa sababu nafanya kitu ambacho nilikuwa na ndoto nacho yaani kwahiyo I am happy kwahiyo, alisema Tunda.

“Nafanya kwa Chidi Benz kama brother yangu kwamba namfeel kitambo, ni brother yangu ambaye sitaki kumuona anakata tamaa kwenye music na bado anajua katika wasanii wa hip hop Chidi Benz is number one . Ni mtu ambaye hata akifanya show hivi yaani audience inakuwa inakubali kitu anachokifanya. Mimi pia nasimamiwa na watu lakini mimi nimejitolea kumsimamia Chidi Benz kwasababu Chidi is my favorite artist Tanzania, pia Chidi Benz ndio role model wangu kitambo. Kwahiyo Chidi Benz ni mtu muhimu sana kwangu na sitaki kuona anapotea au anakata tamaa.”

Pia Tundaman anakiri kuwa bila Chidi Benz asingekuwa hapo alipo leo, “Chidi Benz ni brother yangu ambaye muda mwingi sana alinisupport. Bila Chidi Benz nisingekuwa Tundaman kama sasa hivi.”

Unaweza kutembelea blog ya Tundaman ili kupata habari zake http://www.tundamanbongoflava.blogspot.com/

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents