Michezo

Tyson Fury atangaza kujiuzulu

Bingwa wa ngumi uzani mzito duniani Tyson Fury kutoka nchini Uingereza, ametangaza kujiuzulu ujumbe huo ambao aliuandika katika mtandao wa Twitter.

390e7d9b00000578-3819612-image-a-48_1475496836153

38f8194200000578-0-fury_originally_tweeted_on_monday_morning_to_say_he_was_retiring-a-14_1475519915373

Fury mwenye umri wa miaka 28,alijiondoa katika pigano la marudiao dhidi ya raia wa Ukrain Wladmir Klitschko,lililopangwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na maswala ya kiafya.

Fury ambaye anamiliki mataji ya WBA na WBO anakabiliwa na kesi mnamo mwezi Novemba inayohusisha madai ya utumiaji wa sawa za kusisimua misuli.

”Ndondi ni kitu kibaya zaidi nilichoshiriki”,ilisema Twitter yake akiongezea: ”Mimi ndio bingwa ,na aliyestaafu”

Fury alitarajiwa kupata kitita kikubwa tangu alipojiunga na ndondi wakati wa pigano lake la pili dhidi ya Klitschko katika uwanja wa Manchester mwezi huu.

Aliahirisha pigano la marudio dhidi ya raia huyo wa Ukrain ,ambalo lilipangwa kufanyika mnamo mwezi Julai baada ya kupata jereha la kifundo cha mguu wakati wa mazoezi.

Shirikisho la ndondi duniani WBO limempa siku 10 na kutoa maelezo na kuahirishwa kwa pigano hilo la marudio kwa mara ya pili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents