Michezo

UEFA yaifungulia kesi klabu ya Manchester United

Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limeifungulia kesi ya utovu wa nidhamu klabu ya Manchester United kutokana na kitendo chao cha kuchelewa kufika uwanjani wakati wa mechi yao ya Champions League dhidi ya Valencia hapo jana siku ya Jumanne.

Basi lililobeba kikosi cha United lilichelewa kufika katika uwanja wa Old Trafford kwa mujibu wa ratiba hali iliyopelekea mchezo huo wa kundi H kusogezwa mbele kwa dakika tano.

Polisi wagoma kukisindikiza kikosi cha Man United, Mourinho aipongeza UEFA na mwamuzi kwa huruma yao

Gari hilo la wachezaji lilitoka Lowry Hotel majira ya 6pm lakini lilichukua dakika 75 hadi kufika kwenye uwanja huo ambao upo umbali wa maili tatu kutoka walipokuwa.

Kwa mujibu wa sheria za UEFA, aina hiyo ya kosa hulimwa faini ya euro 10,000  au pauni 8,879 huku meneja wa klabu husika akikosa mechi moja.

Hata hivyo mapema mchana wa leo meneja wa United, Mourinho amewatupia lawama askari polisi wa jiji la Manchester kwa kushindwa kutoa msaada wao wa kulisindikiza basi lililobeba wachezaji jambo ambalo limesababisha kuchelewa kufika uwanjani kwa wakati.

Wakati polisi wakijibu tuhuma hizo wamesema kuwa hakuna ulazima wa kila mechi kupewa ‘escort’ na hata United walishapewa taarifa mapema miezi michache iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents