Michezo

Uingereza yaja na mpango wa kupunguza wachezaji wa kigeni, klabu 20 za PL zakutana kwa majadiliano

Klabu zinazoshiriki ligi kuu Uingereza zinakutana kujadili maombi ya chama cha soka FA, juu ya kuhitaji kupunguzwa kwa idadi ya wachezaji wa kigeni ndani ya timu.

Kwa hivi sasa klabu za ligi kuu Uingereza zina hadi ya wachezaji 17 wakigeni ndani ya kikosi cha wachezaji 25, hivyo FA imekuja na mpango huo ambao itashuhudia wachezaji hao wakipunguzwa kufikia 12 na wazawa kuongezwa hadi kufikia 13.

Katika mkutano huo unaofanyika leo siku ya Jumanne jumla ya klabu 20 zitafikiria wazo la FA kuhusiana na kupungwa kwa idadi ya wachezaji pamoja matumizi ya VAR kwenye ligi hiyo.

Msemaji wa Chama cha Soka Uingereza FA, ameiyambia Sky Sports News kuwa wanaendelea kufanya kazi na klabu za ligi kuu, EFL na mpangilio wa Serikali ikijumuisha DCMS.

Taarifa kutoka ‘Premier League’ zinasema “Kama zilivyo mashirika mengine hutegemea mchanganyiko wa vipaji vya ndani na Kimataifa , bado tunasubiri kufahamu zaidi hali ya kisiasa na udhibiti wa makazi baada ya UK itakapo ondoka kwenye umoja wa Ulaya.”

Ligi Kuu pia ilitoa tamko hilo, ambalo lilisema hivi: “Kama mashirika mengine mengi yanategemea mchanganyiko wa talanta ya ndani na ya kimataifa, tunasubiri kuelewa vizuri zaidi mazingira ya kisiasa na ya udhibiti baada ya Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya.

“Upatikanaji wa vipaji vya soka kwenye pembe zote za Ulaya imekuwa na umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Ligi Kuu, na mahudhurio ya mechi na maslahi ya kimataifa yanaongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wachezaji waliyobora Uingereza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents