Michezo

Ujerumani watuma salamu za vitisho kuelekea kombe la dunia nchini Urusi

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ujerumani jana usiku wameitwanga timu ya taifa ya Saudi Arabia goli 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki kuelekea michuano ya kombe la dunia inayoanza kutimua vumbi alhamisi ijayo.


Magoli ya Ujerumani yamefungwa na Timo Werner na Omar Hawsawi aliyejifunga mwenyewe huku Saudia goli lao likifungwa na Taisir Al-Jassim.

Kwenye mchezo huo, Nahodha Manuel Peter Neuer alitolewa na kuingizwa kipa wa Barcelona, Marc-André ter Stegen dakika chache baadae baada kuingia aliokoa mkwaju wa penati.

Kwenye mchezo huo ambao Ujerumani ilionekana kuutawala mpira katika vipindi vyote viwili inaonesha picha kuwa huenda mwaka huu wakanyanyua tena kombe la dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents