Michezo

Ujerumani yatinga nusu fainali ya Euro 2016

Timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Uero inayoendelea huko nchini Ufaransa baada ya kuifunga timu ya Italia.

img_0154

Ujerumani ambao ndiyo mabingwa wa kombe la dunia walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Italia kwa jumla ya penalti 6-5.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimeshafungana goli 1-1 huku Ujerumani wakiwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 65 lililofungwa na Mesut Ozil, lakini dakika ya 78 Leonardo Bonucci aliisawazishia timu yake ya Italia bao hilo kwa njia ya penalti ndipo zikaongezwa dakika 30 hata hivyo hazikuweza kufungana tena.

1467492667747_lc_galleryImage_Italy_s_Giorgio_Chiellini

Mchezo huo ulionekana kuwa na penalti nyingi zikiwa ni jumla ya penalti 18, Ujerumani walikosa jumla ya penalti tatu nao Italia wakikosa penalti nne.

1467489598829_lc_galleryImage_German_supporters_cheer_d

Wachezaji wa Ujerumani waliokosa penalti ni pamoja na Thomas Muller, Mesut Ozil na Bastian Schweinsteiger huku kwa upande wa Italia wachezaji waliokosa penalti ni Matteo Darmian, Simone Zaza, Leonardo Bonucci n
a Graziano Pelle.

Sasa Ujerumani atakutana na mshindi wa mechi ya leo kati ya wenyeji Ufaransa na timu ya taifa ya Iceland.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents