Habari

Ununuzi wa ndege wakosolewa na Halima Mdee, ‘Tunakwenda kumwaga fedha chini’

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameikosoa vikali serikali kufuatia kutenga Tsh. Bilioni 495 bilioni kununulia ndege mbili.

Wakati akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizaya ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19 leo Bungeni, Mdee amesema hata taarifa za Msajili wa Hazina mwaka 2015/16, zinaeleza wazi kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) halina mpango wa biashara wala wataalamu.

“Hoja si kupinga ununuzi wa ndege, hoja ni fedha hizi za ununuzi wa ndege zitazalisha au tunazipoteza. Taarifa ya ATCL inaeleza wazi kuwa haikuwa na mpango wa biashara. Yaani tunawekeza fedha katika shirika ambalo halina mpango wa biashara,” amesema.

“Shirika lina madeni lakini tunanunua ndege hizi. Bunge litekeleze wajibu wake. Hivi kilimo kinachoajiri Watanzania wengi tunakiwekea fedha kidogo lakini kwenye ndege ambazo tunajua tunakwenda kumwaga fedha chini tunawekeza Sh1 trilioni.” amesisitiza.

Katika bajeti ATCL imetengewa Tsh. Bilioni 495 kununua ndege mbili; moja aina ya Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na ndege kubwa ya masafa marefu aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner), yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents