Habari

Updates: Kaka mkubwa wa marehemu kusafiri leo kuufuata mwili wa Mangwea Africa Kusini

Habari zilizopatikana muda huu zinasema kuwa familia ya Mangwea inajipanga kutuma ndugu kwenda Africa Kusini leo (May 29) kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili wa Marehemu Albert Mangwea.

1

Akiongea na Bongo5 muda mfupi uliopita dada wa marehemu aitwaye Evelyn, amesema kuwa anahitajika ndugu wa marehemu asafiri kwenda Africa Kusini kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili, sababu kule hawawezi kumtoa na kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kwenda.

Kwa Mujibu wa Evelyn familia iko katika mipango ya mwisho ya safari hiyo ambayo kaka yao mkubwa na Mangwea ndiye anayetarajia kusafiri leo hii (May 29) kwenda South Africa kuufuata mwili.

“Habari mpya ni kwamba mtu atoke hapa Tanzania aende akachukue mwili kule hawawezi kuconfirm yaani kumtoa kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kutoka huku, kwahiyo ndio process zinafanywa, kaka yake mkubwa ambaye ni kaka yetu atoke hapa aende South, ndio nadhani atarudi na huo mwili. Ataondoka leo hii hii muda wowote na wakati wowote, “Alisema dada wa marehemu Albert Mangwea.

Msiba wa rapper kipenzi cha wengi Ngwea uko Mbezi Beach Goigi kwa baba yake mdogo , ukishuka goigi ukiulizia kwa mzee Mangwea kwenye msiba utaelekezwa. R.I.P

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents