Mitindo

Urembo wa nywele za Asili

Ukizungumzia suala la kwenda na wakati basi huwezi kuacha kutaja suala zima la nywele hasa nywele za asili zinavyoshika kasi. Karibu katika habari za mitindo hapa Bongo5.

Miaka ya 2000 ilikuwa iliuonekane ni mtu anayekwenda na wakati basi lazima uwe umeweka dawa nywele zako, hali iliyowafanya wadada wengi na wanawake watafute mbadala kwa kuamua kuvaa mawigi licha ya kuwa kwa sasa mawigi ni moja ya kitu muhimu pia kwa mwanamke mrembo kuwa nacho.

Kwa sasa nywele za asili ni moja ya jambo linalozingatiwa na wanawake wengi sana, kwani wameamua kuachana na suala la kutumia dawa za kurainisha nywele.

KWA NINI NYWLE ZA ASILI:
 Mitindo ya nywele za asili imekuwa ikishamiri upaya kwa kipindi hiki na wengi wao wanatumia mitindo hiyo kwa sababu nywele zao hukua kwa haraka.
 Nywele za asili zimekuwa aina ya nywele zisizohiji kutumia pesa nyingi kuzitengeneza. Mfano:- Kusuka na kuosha.
 Usukaji wa nywele umekuwa ni kitu kinachobamba sana kwa sasa . Kati ya wanawake 10 basi sita kati yao wanatunza nywele zao kwa njia ya asili.

HITIMISHO:

Ili tuepukana na suala la magonjwa ya kansa tunashaurisa kutunza nywele zetu kwa njia ya asili.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents