Michezo

Urusi yaipiga kipigo kibaya Saudi Arabia mchezo wa ufunguzi kombe la Dunia

Mwenyeji wa michuano ya kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya timu ya taifa ya Saudi Arabia mchezo wa ufunguzi uliyopigwa hii leo siku ya Alhamisi.

Urusi imejipatia mabao yake matano kutoka kwa wachezaji, Yury Gazinsky aliyetupia dakika ya 12, Denis Cheryshev akitupia dakika ya 43, 90+1, huku Artem Dzyuba akifunga dakika ya 71 na Aleksandr Golovin akihitimisha karamu hiyo ya mabao dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika.

Mpaka sasa hakuna timu yoyote mwenyeji iliyowahi kupoteza mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe na timu ya taifa ya Urusi imeendeleza utamaduni huo baada ya kuibuka na ushindi huo mnono dhidi ya Saudia mchezo wa kundi A.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents