MichezoUncategorized

Usain Bolt kutaja timu aliyosaini kuichezea Jumanne hii, Arsenal, Man United zatajwa

Unadhani Usain Bolt atasajiliwa na timu gani tangu atangaze kujiunga na mchezo wa soka? Mwanariadha huyo mstaafu mwenye rekodi ya dunia, amesema kuwa Jumanne hii ya February 27 atatangaza timu aliyosaini kuichezea.


Usain Bolt akiwa katika mazoezi na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi uliopita

Bolt ambaye anafahamika kuwa ni shabiki mkubwa wa Manchester United, amesema hayo kupitia video ambayo almeiweka kwenye mitandao yake ya kijamii.

“I’ve signed for a football team! Find out which one this Tuesday,” amesema Usain Bolt kwenye video hiyo.


Bolt akiwa katika uwanja wa Old Traford akiangalia moja ya mechi za Manchester United

Mwishoni mwa mwezi January mwaka huu Bolt alionekana akifanya mazoezi na mabingwa wa kombe la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2016, Mamelodi Sundowns.

Baadhi ya mashabiki wameanza kutabiri timu ambayo atajiunga nayo ambapo wamezitaja timu za Arsenal, Manchester United, Dortmund na Real Madrid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents