Michezo

USAJILI: Alikiba akamilisha usajili wa kucheza ligi kuu Tanzania Bara

USAJILI: Alikiba akamilisha usajili wa kucheza ligi kuu Tanzania Bara

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga umethibitisha kukamilisha usajili wa msanii wa muziki wa Bongo, Alikiba kwaajili kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha Sports HQ kinachorushwa na EFM Radio, Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union,Steven Mguto amekiri kukamilika kwa usajili huo hapo jana ambapo dirisha la usajili lilifungwa rasmi.

”Tunashukuru Mungu tumemaliza na tunajaribu kupata wachezaji wote tuliyo wahitaji, Alikiba pia tunaye tumekamilisha usajili wake,” amesema Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union,Steven Mguto.

Usajili: Alikiba kucheza ligi kuu msimu ujao

Alikiba anayetamba na kibao chake cha Mvumo wa Radi ataweza kuisaidia Coastal Union licha ya uchezaji ndani ya uwanja lakini pia ataweza kuibeba klabu hiyo kupitia umaarufu wa staa huyo wa muziki nchini na bara zima la Afrika.

Klabu ya Coastal Union imepanda rasmi ligi kuu mwaka huu baada ya kuiyaga michuano hiyo msimu wa mwaka 2015/16.

Related Articles

4 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents