Michezo

USAJILI: Countinho In, Iniesta Out Barcelona (+Picha)

Chombo cha habari cha Sportsmail kilikuwa cha kwanza kuandika uhamisho wa mchezaji Philippe Coutinho kutua Barcelona kuchukua nafasi ya mkongwe na mwenye mafanikio makubwa ndani ya timu hiyo, Andres Iniesta.

Picha ikimuonesha Philippe Coutinho akiondoka Liverpool wakati timu hiyo ikiwa katika mazoezi

Coutinho raia wa Brazili amependekezwa na Barca kurithi mikoba ya mkongwe Iniesta ambaye amesaini mkataba wa muda mfupi ndani ya Nou Camp.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili inaonekana huwenda akakamilisha usajili wake wa kujiunga na Barcelona baada ya kushindwa kufanya hivyo majira ya joto 

Endapo Countinho atawasili ndani ya klabu hiyo katika kipindi cha dirisha hili la usajili la mwezi huu wa Januari au lile la kipindi cha majira ya joto itakuwa moja ya usajili mkubwa katika Laliga.

Vichwa vya habari vya magazeti ya nchini Hispania, vimeandika kuwa dili la usajili wa mchezaji huyo limefikia hatua za mwisho wa kati gazeti la Mundo Deportivo likiandika katika kichwa cha habari kuwa Coutinho anauwezo wa kucheza zaidi ya nafasi nne

Endapo Barcelona itatoa kitita cha paundi milioni 133 kwa Liverpool basi bila shaka Countinho atatua ndani ya klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili wa mwezi Januari.

Kuwasili kwake Barcelona ni ishara tosha kuwa ndiyo mwisho wa ‘ iconic’ wa timu hiyo, Andres Iniesta

Hivyo Iniesta atashiriki michezo yote ya European na ile ya ligi kabla au baada ya klabu bingwa, Coutinho atachukua nafasi ya kiungo akiwa sambamba na Sergio Busquets na Ivan Rakitic au Paulinho.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents