Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania haitakuwa na uwezo wa kumnunua, Philippe Coutinho kutoka Liverpool iwapo watafanikiwa kumsajili, Ousmane Dembele mwenye umri wa maiaka 20, akitokea Borussia Dortmund, (BBC Radio 5 Live)

Mchezaji, Philippe Coutinho kutoka Liverpool

Barcelona wapo tayari kuwapa Liverpool, Ivan Rakitic kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Philippe Coutinho. (Don Balon)

Barcelona wanamtaka kiungo mchezeshaji wa Real Madrid Marco Asensio na wapo tayari kutoa pauni milioni 72. (Diario Gol)

Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Lexy anakabiliwa na sekeseke la wachezaji kudai kuongezewa mishahara baada ya beki, Danny Rose kushutumu sera za klabu hiyo. (Daily Mirror)

Danny Rose alipokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake baada ya kuweka wazi mtazamo wa Tottenham, huku wachezaji wengine wakitishia na wao kuweka mambo hadharani. (Daily Mirror)

Tokeo la picha la Danny Rose

Mchezaji, Danny Rose

Wachezaji nyota wa Tottenham wanataka  kuondoka kwa sababu ya sera ya malipo ya klabu hiyo. (Daily Mail)

Arsenal wamempa, Alexis Sanchez mkataba mpya na mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uingereza  (Daily Mail)

Juventus wanajiandaa kutoa pauni milioni 23 kujaribu kuishawishi Liverpool kumuuza,  Emre Can. (Gazzetta dello Sport)

Juventus nao wameingia katika mbio za kutaka kumsajili, Sergi Roberto kutoka Barcelona, ambaye pia Manchester United na Chelsea zinataka hudumaye. (Sport.es)

Tokeo la picha la Sergi Roberto

 Mchezaji, Sergi Roberto wa Barcelona

West Ham wamepanda dau la pauni milioni 27.1 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho mwenye umri wa miaka  25. (Daily Telegraph)

Real Madrid wamekuwa na mazungumzo ya siri na Juventus kuhusiana na mshambuliaji Paulo Dybala, 23, ambaye pia anasakwa na Barcelona. (Don Balon)

Juventus wanamtaka, Kevin Strootman kabla ya dirisha la usajili kufungwa, huku Roma wakisema bei yake ni Euro milioni 45. (Tuttosport)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anahitaji huduma ya  beki wa Tottenham, Danny Rose (Daily Record)

Meneja wa Everton, Ronald Koeman ameiambia Tottenham kuwa hawataweza kumsajili kiungo, Ross Barkley kwa bei rahisi. (Daily Star)

PSG wapo tayari kuwapa Atletico Madrid, Javier Pastore katika mkataba wa kumsajili kipa, Jan Oblak mwenye umri wa miaka 24. (AS)

By Hamza Fumo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW