Burudani

Beka Flavour afichua ishu ya kuimba chini ya Polisi

Msanii wa Bongo Flavour, Beka Flavour amedai aliposhikiliwa kituo cha polisi kwa mashtaka ya kutapeli kupitia mtandao alikuwa akiwaimbia washtakiwa ‘mahabusu’ wenzake aliowakuta kituoni hapo.

Kati ya July 19/20 mwaka huu muimbaji huyo alishikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi Tabata Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli Tsh. milioni nane kupitia mtandao wa facebook ambapo baadae alitolewa kwa dhamana.

Beka amekiambia kipindi cha Leo Tena Cha Clouds Fm kuwa ilibidi awaimbie ili kuwaridhisha kwa sababu walitaka lakini kikubwa alichogundua kuna ambao wanatamani kufanya muziki na nyimbo tayari wapo nazo.

“Mule kunakuwa na wasanii wengine, anakuambia dah!, mimi mwenyewe naimba nikitoka humu tu nafanya ngoma yangu, kuna mmoja aliniambia mimi nimejifunza sana nimeshaandika ngoma kwa ajili ya mazingira ya huku ndani nikamuambia hongera ukitoka karekodi ukitoka inaweza ikakutoa,”  amesema na kuongeza.

“Ukigoma wanaweza wakakufanya kitu kibaya kwa sababu wapo wengi halafu wote ni wahuni, kwa hiyo ukileta ubishi wanaweza wakakubadilikia wote,” amesisitiza.

Kwa sasa Beka ameachia wimbo mpya Sikinai baada ya kufanya vizuri na ngoma ya Libebe.

By Pete Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents