Michezo

Ushindi wa Sweden wamuweka pabaya bingwa mtetezi wa kombe la dunia

Bila ya mchezaji wake, Zlatan Ibrahimovic timu ya taifa ya Sweden inafanikiwa kuifunga Korea Kusini bao 1 – 0 mchezo wa kombe la Dunia linaloendelea huko nchini Urusi na hivyo kuiweka kwenye hali mbaya Ujerumani ambayo imepoteza kwenye mchezo uliyopita dhidi ya Mexico.

Bao pekee la Andreas Granqvist lililopatikana kwa njia ya penati dakika ya 65 imeiwezesha timu hiyo kuondoka na alama hizo tatu na kuifanya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa dunia.

Sweden iliyopo kundi F inajipatia pointi tatu na kushika nafasi ya pili sawa na Mexico iliyo duwaza ulimwengu baada ya kuifunga Ujerumani bao 1 – 0 ambaye ni bingwa mtetezi kwenye mchezo wao wa awali.

Kwa namna yoyote mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya taifa ya Ujerumani watalazimika kushinda kwenye mchezo wake ujao wa tarehe 23 ya mwezi huu dhidi ya Sweden ili kujihakikisha nafasi ya kuendelea kutetea taji hilo kwa mwaka huu 2018 wakati Mexico wakiwakabili Korea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents