Michezo

Uwanja wa Uhuru wajaa maji, Yanga yaomba radhi  mashabiki, yavunja mchezo wake dhidi ya Pan Africans

Mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam zimepelekea kughairishwa kwa mchezo wa kirafiki baina ya timu ya Yanga dhidi ya Pan Afrikan uliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Image result for Yanga vs Pan Africans

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema kuwa mechi hiyo imeghairishwa kutokana na uwanja wa Uhuru ambao ungetumika kwa mchezo huo kujaa maji.

”Kutokana na hali ya uwanja wa Uhuru kujaa maji, mchezo wetu dhidi ya Pan Afrikans umeghairishwa. Taratibu zingine zitatangazwa hivi punde. Tunaomba radhi kwa wapenzi na mashabiki wetu kwa usumbufu uliyojitokeza.” imesema Yanga SC.

Hata hivyo Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na visiwa vya Pemba na Unguja.

https://www.instagram.com/p/B3rg1SpA09B/

Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA, Imesema kuwa mvua kubwa itanyesha siku mbili yaani Alhamisi Oktoba 17 na Ijumaa Oktoba 18, 2019 hivyo wananchi wachukue tahadhari na mvua hizo.

Madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na watu kuchelewa kazini, Na kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents