DStv Inogilee!

Vaa High Heels kwa kujiongeza

Natumaini uko salama kabisa, nakukaribisha katika ulimwengu wa mitindo kutoka hapa Bongo5, na leo tutazungumzia juu ya uvaaji wa kiatu kirefu maarufu kama High Hills, aina hii ya kiatu huvaliwa na wanawake wengi ila wengi wao hujikuta wanavaa bila kujua kwanini wanavaa.

High hills huvaliwa na wanawake wote hasa ukijulia ni kisigino gani kitaendana na mwili wake, ni ajabu sana kumkuta mwanamke mwenye mwili mkubwa akivaa kiatu kirefu chanye kisigino chembamba, kwani kinaweza kuzidiwa kutokana na mwili na kupelekea kukatika.

Ni vizuri kujua aina ya mwili wako ili uendana na kiatu unachotakiwa kukivaa, sio sawa mtu mwenye mwili kuvaa kiatu kilicho na kigizo cha kukuhaibisha pia sio vyema kuvaa kiatu kikubwa ilimradi tu uendane na wakati wa hicho kiatu. Kabla hujanunua sio dhambi kujaribisha ukiwa dukani ama kupitia kiatu hicho katika mtandao ujue kinatakiwa kuvaliwa na mtu wa aina gani yaani mwili pamoja na umri.

Na Laila Sued.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW