MichezoMitindo

Van Persie arejea timu yake iliyomkuza Feyenoord

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin Van Persie amerejea katika timu yake ya zamani iliyomkuza ya Feyenoord na kusaini mkataba wenyethamani ya paundi milioni 1.5 kwa mwaka akitokea Fenerbahce kwa uhamisho huru.

 

Van Persie ameripoti hii leo De Kuip ili kukamilisha uhamisho huo  wa kurejea  Feyenoord tangu ipite miaka 14 toka kuondoka kwake na kujiunga na  Arsenal 2004 akiondoka hapo mwaka 2002.

Miongoni mwa klabu alizopata kuchezea Van Persie  kabla ya kurejea tena katika ligi ya Uholanzi ni the Gunners , Manchester United na Fenerbahce.

Van Persie akisaini mkataba leo siku ya Jumatatu na atavaajezi namba  32.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents