Michezo

Video iliyomnasa Alves akipenga makamasi na kumpangusia Ronaldo yazua gumzo

Mchezaji bora duniani anaekipiga klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameingia katika gumzo kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani baada ya kuenea kwa video inayomuonyesha akifutiwa makamasi na mchezaji, Dani Alves wakati wa mechi yao dhidi ya Paris Saint-Germain iliyokwisha kwa mabao 2 – 1 michuano ya klabu bingwa bbarani Ulaya siku ya Jumanne.

https://youtu.be/eyg_rjty_64

Mjadala mkubwa ni kitendo cha Alves mchezaji wa kimataifa wa Brazili kufuta makamasi kwa kutumia mkono wake kisha kumfutia Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa dunia.

Kabla ya kitendo hicho kumekuwa na patashika kati ya wachezaji hao wawili hali iliyopelekea Ronaldo kumpiga teke kwa makusudi Alves.

Alves ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Barcelona kwa miaka tisa huku akiwa na historia na Ronaldo tangu siku ya kwanza anakabiliana naye katika ligi ya La Liga amekuwa na ushindani naye kwa kipindi chote hicho.

Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka huu Alvesi amesema kuwa anamuheshimu sana Ronaldo tofauti na vyombo vya habari vinavyo andika.

Vyombo vya habari ndiyo vinavyo andika kuwa nina ugomvi na Cristiano.

Laiti watu wangefahamu kwa kiasi gani namheshimu sana Cristiano Ronaldo naliweka sawa hili narudia tena namheshimu sana Cristiano Ronaldo.

Kilamtu ananiambia kwakiasi gani alivyo kuwa na kipaji kama Ronaldo,ni tofauti kwangu nilipaswa nishindane naye.

Dani Alvesi akimsukuma Ronaldo wakati akiwa na klabu yake ya Barcelona

Mitandao mingi ya michezo imeandika na kuposti video hiyo inayo muonyesha Dani Alves akifanya kitendo hicho wakati wa mchezo wao dhidi ya Madrid.

 

https://twitter.com/DaniAlvesD2/status/971708270669959168

Ningumu katika taaluma yangu mara nyingi hauwezi kuepuka, hii ni sehemu ya maisha yetu kusikia na kuona vitu kama hivi.

Nitaendelea kupambana kama nilivyo fanya hadi hii leo.

https://twitter.com/DExpress_Sport/status/971717810744381441

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents