MichezoUncategorized

Video: Kuna maisha baada ya soka, Ronaldo ampa heshima yake Gianluigi Buffon wa Juventus

Nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonyesha heshima yake kwa mlindalango wa timu ya Juventus, Gianluigi Buffon baada ya kumsalimia kwa bashasha wakati akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari muda mchache tu toka staa huyo raia wa Ureno akiadhibu kibibi cha ‘Turin’ kupitia mkwaju wa penati na kujihakikishia kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Mlindalango, Gianluigi Buffon amjia juu mwamuzi, Michael Oliver kwa kuipa Real Madrid penati (+Picha)

Ronaldo amekutana na Buffon na kusalimiana baada ya nyota huyo wa Madrid kuondoka Bernabeu usiku wa siku ya Jumatano.

Buffon ambaye ni kipa wa muda mrefu wa klabu ya Juventus ya Italia hapo jana alikuwa mwiba mkali mbele ya mwamuzi wa Uigereza, Michael Oliver kwa kuchukizwa na kitendo chake cha kuwapatia Real Madrid penati dakika ya 93 ya mchezo ambayo kwa upande wake aliona haikuwa sahihi kitendo ambacho kilimpelekea kupewa kadi nyekundu na kutoka nje.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents