Michezo

Video: Liverpool yaendeleza ubabe EPL, mlindalango wake aingizwa kwenye vitabu vya reko kwa bao hili

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Leicester mchezo wa ligi kuu England.

Liverpool imefanikiwa kupata ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake Sadio Mane akifunga bao la kwanza dakika ya 10 na Firmino  akiweka kambani la pili dakika ya 45 huku Leicester wakipata lakufutia machozi kutokana na uzembe wa mlindalango wa Liverpool, Alisson Ramses Becker akitaka kumpiga chenga, Ghezzal kisha mpira kumshinda na mchezaji huyo kuandika bao hilo dakika ya 63.

Kwa matokeo hayo Liverpool anaongoza ligi kuu England kwa kuwa na jumla ya pointi 12 akishinda michezo yake yote minne akifatiwa kwa karibu kwenye msimamo na Tottenham wenye alama tisa wakiwa wamecheza mechi tatu.

Liverpool inafanikiwa kuweka historia kwa kushinda jumla ya michezo minne ya ufunguzi wa ligi kuu England tangu ilivyofanikiwa kufanya hivyo msimu wa mwaka 1990/91 ikiwa chini ya Kenny Dalglish.

Wakati kiungo wake, James Milner akifanikiwa kufikisha jumla ya ‘assists’ ikiwa ni idadi sawa na aliyowahi kuiweka, David Beckham.

Kikosi cha klabu ya Leicester: Schmeichel (6), Ricardo Pereira (5), Morgan (5), Maguire (5), Chilwell (8), Mendy (6), Ndidi (8), Albrighton (6), Maddison (8), Gray (6), Ghezzal (7)

Wachezaji wa akiba: Amartey (6), Iheanacho (7), Okazaki (6)

Kikosi cha klabu ya Liverpool: Alisson (6), Alexander-Arnold (6), Gomez (9), van Dijk (7), Robertson (7), Wijnaldum (6), Henderson (6), Milner (6), Salah (6), Firmino (7), Mane (7)

Wachezaji wa akiba: Matip (6), Keita (6), Shaqiri (6)

Mchezaji bora wa mchezo huo ni Joe Gomez

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents